Luis Figo amesema "soka            limepotea" baada ya Sepp Blatter kuchaguliwa tena kuwa rais wa            Fifa jana na kumtaka kwa mara nyingine tena kuondoka katika            nafasi hiyo.
        Blatter (79) alimshinda            mpinzani wake Prince Ali kutoka nchini Jordan, ambapo sasa            atakaa tena madrakani kwa miaka minne mingine huku akiwa            amekaa madarakani kwa takribani vipindi 5.
        Blatter alipata kura 133            dhidi ya 73 za Prince Ali kabla ya mpinzani wake huyo kuamua            kujitoa katika raundi ya pili.
        Ushindi wake umekuja huku            viongozi 14 wa shirikisho hilo wakiwa wamekamatwa kwa tuhumu            za rushwa siku chache tu kabla ya uchaguzi.
        Figo – ambaye hapo awali            alipanga kuwania nafasi hiyo kabla ya kujitoa kwa madai ya            kutozigawa kura ili kurahisisha kumng'oa Blatter, amesema kuwa            amehuzunishwa sana na matokeo ya uchaguzi huo.
        "Leo ilikuwa ni siku            nyngine ya giza hapa Zurich," alisema nguli huyo wa Ureno.            "Fifa imepotea, lakini juu ya yote hayo, soka limepotea na            kila mpenda soka amepotea pia.
        "Blatter alitoa sababu za            kijinga sana pale aliposema hawezi kudhibiti kila mtu ndani ya            shirikisho. Hilo ni kama tusi kwa wapenda soka. Hawa watu,            ambao Blatter amekuwa akiwatunuku vyeo kwa miaka kadhaa, leo            anawageuka, Fifa sio shirikisho lenye maadili tena.
        "Kama Blatter alihusika            kwa udogo katika soka, basi sidhani kama angechaguliwa. Kama            ana upungufu wa maadili, basi ndani ya miaka michache ijayo            atajiuzulu."
        
Comments
Post a Comment