LIVERPOOL BADO YAMPIGIA HESABU JAMES MILNER ILI AWE MRITHI WA STEVEN GERRARD


LIVERPOOL BADO YAMPIGIA HESABU JAMES MILNER ILI AWE MRITHI WA STEVEN GERRARD

Liverpool bado inadaiwa iko mawindoni kwenye dili la kumsainisha staa wa Manchester City, James Milner anayetakiwa 'kuvaa viatu vya Steven Gerrard' katika dimba la kati.
Staa huyo wa kimataifa wa England anatarajiwa kuwa mchezaji huru kiangazi hiki wakati mkataba wale na City utakapokoma, na mazungumzo ya kuuongeza yakikwama.
Arsenal pia inahusishwa na uhamisho wa staa huyo mwenye umri wa miaka 29, lakini sasa taarifa zinasema Liverpool ndiyo yenye nafasi kubwa ya kupata saini yake.
Taarifa zinadai zaidi kuwa kituo kipya cha Milner ni Anfield – licha ya kuwa City inatarajiwa kuweka ofa ya mwisho ya mkataba mpya kuhakikisha inambakisha.


Comments