KWAHERI STEVEN GERRARD



KWAHERI STEVEN GERRARD

gerrard

Na Anwar Binde.

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amehitimisha uwepo wake ndani ya Liverpool kwa takribani miaka kumi na saba katika hali iliyojawa na hisia kali na huzuni vile vile. Mechi yake dhidi ya Crystal Palace ndo ilikua mechi yake ya mwisho ndani ya uwanja wa Anfield.

Mchezaji huyu mwenye miaka 34 alipewa mapokezi makubwa sana na mashabiki waliofurika uwanjani kuangalia mechi ya mwisho ya Steve Gerrard ndani ya Anfield na ukiwa ni mchezo wake wa 709 kwa Liverpool ambao uliishia kwa kichapo cha 3-1 dhidi ya Crystal Palace

"Kulikua na hisia nyingi sana, pia kuhusu jinsi nilivyoagwa siwezi elezea ni kitu ambacho hakielezeki" alisema Gerrard

"Naridhika nikiangalia miaka kumi na saba nyuma mpaka sasa na sito hisahau siku hii ya leo" aliendelea Gerrard.

Gerrard atacheza mechi ya mwisho dhidi ya Stoke City wikiendi inayokuja, kabla ya kwenda kuichezea L.A Galaxy ya nchini Marekani wakati wa majira ya joto.

Mashabiki wa Liverpool walifika uwanja wa Anfield saa moja kabla ya mchezo kuanza dhidi ya Palace kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa mchezaji wao kipenzi Steven Gerrard. Steven Gerrard alipewa heshima na wachezaji wa timu zote mbili wakati akiingia uwanjani.

Tatizo dogo lililojitokeza ni kua matokeo haya kuendana na tukio nzima kama lilivyokua, baada ya Crystal Palace kupata ushindi wa goli 3-1 japo kua Liverpool ndo walitangulia kupata bao.

Baada ya mchezo kumalizika Gerrard alibaki akiwaaga mashabiki waliosalia kwa ajili ya kumuaaga na vile vile wachezaji wenzie walikua wamevalia fulana zilizokua na namba ya jezi ya Steven Gerrard mgongoni mwao.

"Steven Gerrard amepewa kwaheri iliyostahili kwa hadhi yake na amejitolea kwa kila kitu mpaka mwisho" alisema Brendan Rodgers.

" Lilikua ni jambo nzuri kwake na familia yake kwa ujumla lakini ndo hivyo tena matokeo ya mchezo na kiwango tulicho kionyesha havikurizisha". Aliendelea Brendan Rodgers

" Steven ni mchezaji na binadamu ambaye hawezi kupatiwa mbadala kwa yale aliyochangia ndani ya klabu hii kwa mda wote aliokuwepo hapa."

GERRARD KATIKA KUREJEA ANFIELD

Gerrard aliulizwa kama kuna uwezekano wa yeye kurudi Liverpool kwa mkopo hapo baadae.

"Nataka niwaage Liverpool vizuri" alisema Gerrard

"Jambo litakalo nifanye nirudi hapa labda liwe la dharura, ila natumai sitahitajika wakati wa majira ya baridi"



Comments