KUELEKEA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA


KUELEKEA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA

uefa

Na Anwar Binde.

Klabu Bingwa Ulaya inaelekea ukingoni ikiwa imebakiza mchezo moja wa fainali utakao zikutanisha klabu ya Barcelona na Juventus. Moja kati ya timu izi mbili ina nafasi ya kuvishwa taji la klabu bora ulaya msimu wa 2014-2015 katika fainali itakayo pigwa tarehe 6 mwezi wa 6. Yafuatayo ni mambo ma 5 unahitaji kujua wakati Spain na Italy zitakapo pambana;

  1. LIONEL MESSI KUFIKISHA 4-0
    Kila mmoja wetu ambaye ni mpenzi na shabiki vile vile mafatiliaji mzuri wa soka anajua ya kwamba Messi ni mchezaji bora kuwai kutokea ama wengine wakidiriki kusema ni bora kuliko waliopita. Japo ana mapugufu yake kama kutoweza kunyakua kombe la Dunia wala lile la Amerika ya Kusini lijulikanalo kama Copa America. Tukirudi Ulaya Messi amekua hatari sana haswa katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya akifanikiwa kunyakua taji hilo mara 3, 2006 akinyakua dhidi ya Arsenal iliyokua ikiongozwa na Henry 14, 2009 na 2011 dhidi ya Manchester United akiweza funga goli la kichwa mbele ya beki mrefu Rio Friednand. Zote hizi zikiwa ni timu kutoka Uingereza, ndani ya fainali hii wachumbuzi na wapenzi wa soka watakua waki subiri kuona kama Messi na Barcelona wataweza kunyakua taji hili dhidi ya timu kutoka Italia na kumfanya Messi kufikisha mataji manne ya Klabu Bingwa Ulaya.
  2. FAINALI ZA WAHISPANIA DHIDI YA WATALIANO
    Kitaifa nchi hizi mbili zina mafanikio makubwa sana, zikifanikiwa kuchukua mataji mbali mbali kwa ngazi ya Taifa, hapa tukizungumzia Mashindano ya Euro na yale ya kombe la Dunia. Kwa upande wa Klabu Bingwa Ulaya timu kutoka Italia zimefanikiwa kubeba taji hili mara 12 ambapo kinara wao akiwa AC Milan waliofanikiwa kubeba mara 7. Wakati kwa upande wa Hispania kinara wao ni Real Madrid akiwa amejinyakulia taji hilo mara kumi na kufanya timu kutoka Hispania kubeba kombe hilo mara 14. Mara ya mwisho kwa timu kutoka italia na Hispania kukutana katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya ni mnamo mwaka 1998 ambapo Real Madrid walicheza dhidi ya Juventus na mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa Real Madrid walitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli moja kwa bila.
  3. GIORGIO CHIELLINI NA LUIS SUAREZ WANAKUTANA TENA

Unakumbuka mchezo wa Kombe la Dunia mwaka 2014 uliowakutanisha Uruguay dhidi ya Italia, katika mchezo huo kulitokea kituko ambapo mchezaji wa Uruguay Luis Suarez alimng'ata Giorgio Chiellin begani na kupelekea Suarez kupewa kadi nyekundu na baadae kupewa adhabu kali ya kufungiwa kucheza soka kwa mda. Katika fainali hii ya Klabu Bingwa Ulaya wanakutana tena huku Chiellini akiwa mchezaji wa Juventus na Suarez akiwa ndani ya jezi ya Barcelona. Suarez ameanza msimu kwa kusua sua lakini amefanikiwa kurudi katika kiwango chake na kufanikiwa kupachika magoli mengi mpaka sasa. Kwa uchambuzi wa haraka haraka tunaona marefa wa mchezo huu watakua makini sana na wachezaji hawa.

  1. MESSI ANAFUKUZIA REKODI YA MCHEZAJI MWENYE MAGOLI MENGI KLABU BINGWA ULAYA
    Messi na Christian Ronaldo wataendelea kupambanishwa kwa vizazi na vizazi, Messi si kwamba tu anasaka taji lake la nne la Klabu Bingwa Ulaya bali pia anataka kuvunja rekodi ya mchezaji mwenye magoli mengi katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya. Messi na Ronaldo wote wako sawa katika magoli waliyofunga wakiwa na magoli 77 kwa kila mmoja. Huu ndo wakati mzuri na mechi nzuri kuvunja rekodi kwa Messi, kama akifanikiwa kufunga hata goli moja atakua juu ya Ronaldo kwa magoli 78 dhidi ya 77 ya Ronaldo japo kuwa amecheza michezo kumi na sita pungufu ya mpinzani wake.
  2. MFALME WA HISPANIA NA ULAYA
    Mpaka sasa ndani ya La Liga ama ligi kuu ya Hispania Barcelona ndo kinara wa ligi ikiwa zimesalia mechi mbili ligi kuisha. Labda yatokee maajabu ya Mussa fimbo ndo Barcelona wanaweza kupokonywa nafasi ya kuwa bingwa kwa mwaka huu. Kunyakua ubingwa wa ligi na hapo hapo kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya ni mafanikio makubwa sana kwa klabu yoyote. Vuta kumbukumbu kidogo juu ya hilo, ni mara 4 tu tangu mwaka 1959 kwa timu kutoka Hispania kuchukua ubingwa wa La Liga na hapo hapo kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya; Barcleona 2011, Barcelona 2009, Barcelona 2006 na Barcelona 1992. Umegundua kitu hapo, miaka yote minne ambayo Barcelona wamefanikiwa kuwa mabingwa wa ulaya wamefanikiwa pia kuwa mabingwa wa ligi ya nyumabani ama La Liga. Mara ya mwisho Real Madrid walifanya hivyo mwaka 1958.

Kwa leo tuweke kituo hapo kesho tureje kwa mengine mengi zaidi zikiwa zimesalia takribani wiki tatu mpaka mtanange wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.



Comments