Kocha Taifa Stars ashukuru kushiriki Cosafa, Makapu kurejea Tanzania leo!


Kocha Taifa Stars ashukuru kushiriki Cosafa, Makapu kurejea Tanzania leo!
thumb_IMG_1356_1024
KOCHA mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij baada ya jana kuchapwa goli 1-0 na Swaziland katika mechi ya ufunguzi ya mechi ya Cosafa ameamua kutoa shukurani kwa kualikwa.
Nooij amesema anashukuru kwa kupata mwaliko huu, kwani kwake anatumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON, CHAN) mwezi juni.
Kocha huyo  anaamini wachezaji aliowaacha majeruhi nyumbani pamoja na wachezaji wa kimataifa wanaochezea klabu ya TP Mazembe, wataongeza nguvu katika kikosi chake watakaporejea Tanzania.
Baadhi ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini walijitokeza uwanja wa Royal Bafokeng kuishangilia timu ya Taifa ya tanznaia Taifa Stars wakiwa sambamba na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili siku ya jumatano saa 11 za jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Madagascar katika uwanja wa Royal Bafokeng., ambao katika mchezo wa awali wamibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho.
Wakati huo huo kiungo wa Taifa Sars Said Juma "Makapu" ambaye anasumbuliwa na majeruhi, anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania leo kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na matibabu.


Comments