Katibu mkuu Simba abwaga manyanga


Katibu mkuu Simba abwaga manyanga

STEPHEN ALLY

KATIBU Mkuu wa Simba, Stephene Ally, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya madaktari wa timu ya taifa ya Muhimbili kumshauri kupumzika kwa muda usiojulikana kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo.

Stephene aliingia madarakani mwaka jana mara baada ya uongozi kuingia madarakani kuiongoza timu hiyo chini ya Rais Evans Aveva.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na kukaririwa na Salehjembe, Stephene amesema kikubwa kilichomfanya ajiuzulu ni kutokana na matatizo ya kiafya.

"Cha kwanza kabisa katika mwili wa binadamu ni afya na hayo mengine yanakuja baadaye, madaktari wamenishauri nipumzike kufanya kazi kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kujiuguza kwanza. Ugonjwa sitaweza kuutaja kwa sasa, tayari nimekabidhi barua kwa uongozi.

"Ninaomba nichukue muda huu kuwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki kwa jumla kwa kipindi chote nilichokuwa ninaiongoza Simba," alisema Stephene.



Comments