Juventus yawapa vidonge vyao waliowabeza…



Juventus yawapa vidonge vyao waliowabeza…
11263923_1139713289389232_9118449485690423068_n
UKURASA rasmi wa facebook wa  Juventus amejibu mapigo kwa wale wote waliokuwa wanawabeza baada ya kufika nusu fainali.
Baada ya droo ya mechi za nusu fainali za Uefa Champions League kutoka, wengi waliwadharau Juventus na kuwaona wanyonge katika timu nne zilizosalia.
Wakicheza nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003, Juventus wamewashangaza wengi baada ya kuwachapa mabingwa watetezi, Real Madrid kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2.
Miamba hiyo ya Italia itakabiliana na Barcelona katika mechi ya fainali juni 6 mwaka huu mjini Berlin na wanatarajia kutwaa ubingwa wa kwanza wa Uefa tangu walipofanya hivyo mwaka 1996.
Ukurasa wa facebook wa Juventus ume-post picha chache leo kuwajibu waliowadharau kabla ya mechi za nusu fainali.
Katika picha hizo waliandika maneno yaliyosomeka ""Remember these?" yaani Unakumbua haya?

14May2015

 


Comments