Juventus imeinyima dunia kile kilichotarajiwa kuwa fainali kubwa kuliko zote za Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimisha sare ya 1-1 kwa Real Madrid.
Hiyo inamaanisha kuwa ndoto ya Real Madrid kukutana na Barcelona kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeyeyuka na sasa ni Juventus wanaopenya kwenda Berlin. Hukuna tena fainali ya Barcelona na Real Madrid wala fainali ya Messi na Ronaldo.
Barcelona ilitangulia fainali baada ya kuitoa Bayern Munich kwa jumla ya bao 5-3.
Ronaldo aliipatia Real Madrid bao la kuongoza dakika ya 23 kwa njia ya penalti na kudumu hadi mapumziko.
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Alvaro Morata alikuwa mwiba kwa mara ya pili kwa wenyeji baada ya kuisawazishia Juventus dakika ya 57.
Alvaro Morata alifunga pia katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita ambapo Juventus ilishinda 2-1.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Sergio Ramos, Varane, Marcelo, Rodriguez, Kroos, Isco, Bale, Benzema, Ronaldo
Illarramendi
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Pogba, Pirlo (Barzagli 79), Marchisio, Vidal, Tevez, Morata (Llorente 84)
Comments
Post a Comment