Hii ndio ‘engo’ mpya ya stori ya Man United kujaribu kumsajili Gareth Bale…



Hii ndio 'engo' mpya ya stori ya Man United kujaribu kumsajili Gareth Bale…
Gareth+Bale+Real+Madrid+CF+v+Juventus+zN1xG7MV5Hbl
MIPANGO ya usajili wa majira ya kiangazi wa Manchester United leo imetawala vichwa vya magazeti mengi  barani ulaya .
Gazeti la Times limeripoti kuwa Man United wameweka rada zao zote kwa nyota wa Spurs, Harry Kane, wakati magazeti mengine matatu yanasema wanataka kumnunua Gareth Bale.
Magazeti ya The Express,  The Mirror na The Star yanadai kuwa United wametenga paundi milioni 80 kumnunua Bale ambaye sasa haizuiliki kuondoka Santiago Barbebeu.
Hakuna wazo jipya juu ya United kumuwinda Bale kwani ilishawahi kufanya hivyo hata kabla ya kutua Real Madrid, lakini The Mirror limekuja na kona nyingine ya Stori likidai mashetani hao wekundu wako tayari kuwauza Angel Di Maria na Robin van Persie ili kuongezea fedha za kumsajili Bale.
Kumuuza Robin van Persie sio ishu kwasababu ya majeruhi yake ya siku za karibuni, lakini kumuuza Angel Di Maria itakuwa stori kubwa kwasababu amecheza mwaka mmoja tu tangu United walipovunja rekodi ya usajili ya soka la Uingereza wakitumia karibia paundi milioni 60 kumleta Old Trafford kutokea Real Madrid.

 



Comments