Liverpool itafanya mazungumzo ya mwisho na mshambuliaji wake Raheem Sterling wiki hii kujaribu kumshawishi nyota huyo asiondoke, huku tayari akiwa ameshamwambia kocha Brendan Rodgers kuwa anataka kutimka Anfield.
Sterling alifanya mazungumzo ya siri na Rodgers kabla ya mchezo wa sare 1-1 na Chelsea na kuweka wazi kuwa hataki tena kubakia Liverpool msimu ujao.
Hata hivyo mchezaji huyo wa kimataifa wa England amekubali kutoa nafasi moja ya mwisho ya kufanya mazungumzo na klabu hiyo.
Sterling amekataa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano akiamini klabu haina uwezo wa kupigania mataji.
Mshambuliaji huyo anataka pia kuendelea kucheza Ligi ya Mabingwa, kitu ambacho hatakipata Liverpool msimu ujao.
Lakini pia Sterling anaona kashushwa thamani kwa dili jipya lililowekwa mezani na Liverpool litakalo mwingizia pauni 90,000 kwa wiki.
Sterling (kulia) amemwambia wazi kocha wake kuwa anataka kutimka Liverpool
Sterling analipwa £35,000 kwa wiki Liverpool, na amebakiza miaka miwili katika mkataba wake
Comments
Post a Comment