Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
UONGOZI wa Mtibwa Sugar FC umesema hatma ya kocha mkuu wao, mzawa Mecky Mexime katika klabu hiyo, itajulikana wakati wa kikao cha bodi ya wakurugenzi.
Msemaji wa Mtibwa Sugar FC, Thobias Kifaru, amesema leo kuwa kikao kijacho cha mabosi wa klabu hiyo ndicho kitaamua kuendelea ama kuachana na nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars.
"Mecky ni kijana wetu, lakini timu haijafanya vizuri katika miaka mitatu aliyokuwa nayo. Kikao cha Bodi ndicho kitaamua hatma yake.
"Tayari Mratibu wa klabu (Jamal Bayser) amesjhazungumza na mmoja wa makocha wa kigeni, lakini ni mapema kusema kitakachotokea. Kikao ndicho kitakachoamua kila kitu," amesema Kifaru.
Mexime, nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar FC, ameshindwa kuifanya timu hiyo kufika katika mafanikio yake ya mwishoni mwa karine iliyopita.
Mtibwa Sugar FC ilitwaa mara mbili mfululizo ubingwa wa Tanzania Bara mara mbili mfululizo 1999 na katika mwaka wa amabadiliko ya karne.
Mexime amedaiwa kushindwa kuwaunganisha wachezaji na wakati mwingine kuwa na migogoro na baadhi yao.
Mwezi uliopita, mmoja wa nyota wa klabu hiyo alidai kuwa Mexime amekuwa na tabia ya kutowapanga kikosini baadhi ya wachezaji wasiompa sehemu ya posho zao.
Comments
Post a Comment