BOSI wa Bayern Munich, Pep Guardiola amemtaja Lionel Messi kuwa ndiye 'mchezaji bora wa wakati wote'.
Guardiola ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kutupwa nje ya UEFA kwa kipigo cha jumla cha magoli 5-3 dhidi ya Barcelona.
Mechi ya kwanza kocha huyo wa zamani wa Barcelona alikufa 3-0 Camp Nou na jana usiku ameshinda 3-2.
Messi amecheza kwa kiwango cha juu katika mechi zote mbili na kumfanya Guardiola ashindwe kuzuia hisia zake.
"Ni mchezaji bora wa wakati wote,' Guardiola amesema. "Namfananisha na Pele. Ninafurahia sana kuona mpira wa aina hii". Amekiri Guardiola.
Nyota huyo ambaye anafurahia msimu mzuri Barcelona na ameshafunga magoli10 katika mashindano ya ulaya, juma lililopita aliwafumua Bayern katika kipigo cha kwanza cha mabo 3-0 Camp Nou akifunga mara mbili.
Comments
Post a Comment