Rapa wa zamani wa Twanga Pepeta na Extra Bongo, Grayson Sesemkwa (pichani juu) amejiunga na Double M Sound ya Mwinjuma Muumin na tayari ameshiriki kurekodi nyimbo mpya za bendi hiyo.
Msanii mwingine aliyejiunga na bendi hiyo ni mwimbaji Bob Kisa ambaye pia aling'ara na Extra Bongo.
Bob Kisa pia ameshiriki kuimba nyimbo mbili "Utafiti wa Mapenzi" na "Nikufaninishe Nani" ambazo ziko studio kwa Amoroso Soundo.
Muumin ameiambia Saluti5 kuwa wasanii hao wataongeza nguvu katika Double M Sound katika kipindi hiki ambacho anajaribu kuisuka upya bendi yake.

Comments
Post a Comment