Winga matata anayeelekea Manchester United msimu ujao, Memphis Depay amefunga kwa free-kick ya ajabu wakati mabingwa PSV Eindhoven walipoitungua Heracles 2-0 katika mechi ya ligi ya Uholanzi siku ya Jumapili.
Nyota huyo wa miaka 21 alikuwa akicheza mchezo wake wa mwisho kwenye uwanja wa nyumbani ambapo akaendelea kujikita kileleni katika orodha ya wafungaji bora kwa free-kick ya aina yake akifikisha magoli 22 ya ligi msimu huu.
Inatosha kabisa kuonyesha ni kwanini United imekubali kumsajili ada inayotajwa kufikia pauni milioni 30 ili kupata huduma yake msimu ujao.
PSV ilipata free-kick ya umbali wa mita 35 dakika ya 32 ambapo Depay aliukwamisha mpira wavuni
Nyota mpya wa Manchester United akipiga mpira wa free-kick na kuifungia PSV
Mpira unapenya ukuta wa Heracles na kwenda wavuni
Kipa alijaribu kuruka lakini alichelewa, tayari mpira wa Depay ulikuwa wavuni
Depay akiwaaga mashabiki wa PSV
Kocha wa PSV Phillip Cocu akimpongeza Depay
Orodha ya wafungaji bora wa ligi ya Holland
| Player | Team | |||
|---|---|---|---|---|
| M. Depay | PSV | 22 | 2 | 6 |
| L. de Jong | PSV | 19 | 2 | 12 |
| M. Kramer | ADO | 17 | 0 | 11 |
| M. Uth | Heerenveen | 15 | 3 | 8 |
| T. Chery | Groningen | 14 | 1 | 8 |
| M. de Leeuw | Groningen | 14 | 1 | 9 |
| B. Ogbeche | Cambuur | 13 | 1 | 6 |
| T. van Weert | Excelsior | 13 | 0 | 9 |
| G. Wijnaldum | PSV | 13 | 0 | 6 |
| A. Tighadouini | NAC | 12 | 2 | 8 |
| N. Gudelj | AZ | 11 | 2 | 6 |
| S. Haller | Utrecht | 11 | 4 | 5 |
| C. Kazim-Richards | Feyenoord | 11 | 1 | 7 |
| A. Milik | Ajax | 11 | 1 | 4 |
| S. Nijland | Zwolle | 11 | 1 | 3 |
Comments
Post a Comment