KITENDO cha Steven Gerrard kuondoka Liverpool hakitakuwa cha kudumu, kwa mujibu wa kocha Brendan Rodgers.
Nahodha huyo, 34, kesho jumamosi atacheza mechi yake ya mwisho Anfield dhidi ya Crystal Palace na baada ya hapo majira ya kiangazi mwaka huu anakwenda kujiunga na La Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani (MLS).
"Ni mtu ambaye ningependa kufanya naye kazi atakapomaliza mpira wake. Fursa ya yeye kurudi ni kubwa kama nitaendelea kuwepo hapa', Amesema Rodgers.
UWEZEKANO WA MKATABA WA MKOPO
Rodgers amesema Gerrard kurudi kwa mkopo wakati wa mapumziko ya ligi ya Marekani inawezekana ingawa bodo hawajafanya mazungumzo.
Siku za nyuma, Mkurugenzi mkuu wa Liverpool, Ian Ayre alisema kumchukua kwa mkopo Gerrard januari mwakani imepokelewa vizuri.
Gerrard ameichezea Liverpool zaidi ya mechi 700 tangu acheza mechi yake ya kwanza mwaka 1998 na ameshinda ligi ya mabingwa, kombe la Uefa, makombe mawili ya FA na makombe matatu ya ligi.
ALAMA YA MJI
"Niliwauliza viongozi wa timu namna wanavyoweza kumuelezea Steven kwa neno moja, watasema neno gani?," Ameongeza kocha wa Liverpool.
"Kitu ambacho Steven amefanya katika mji, hata wanasiasa hawajaweza kuufanyia mji. Yeye ni alama ya ajabu ya mji kwa watu wa hapa na ndiye tunu ya klabu".
MAONI YA KOCHA WA ARSENAL, ARSENE WENGER KUHUSU GERRARD.
"Kwangu mimi ni mchezaji wa ajabu, utumishi wake umetukuka kwa Liverpool katika maisha yake yote ya soka, sio rahisi kuona wachezaji wa aina hiyo".
'Pia kesho ni siku maalumu kwa soka la England kwasababu alikuwa mchezaji mkubwa ndani ya timu ya taifa"
Comments
Post a Comment