FUJO ZA VAN GAAL ZAANZA, MAN UNITED YATUMA MAOMBI KUMSAJILI RAHEEM STERLING ...mwiko wa miaka 51 hatarini kuvunjwa
Manchester United imepeleka maombi ya kutaka kumsajili winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Hakuna mchezaji aliyewahi kukatiza moja kwa moja baina ya timu hizo mbili zenye upinzani wa hali ya juu tangu mwaka 1964 wakati Phil Chisnall alipotoka United na kujiunga na Liverpool.
Hata hivyo Liverpool wameiambia Manchester United kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa England.
Raheem amekataa kusaini mkataba mpya na amemwambia wazi kocha wake Brendan Rodgers kuwa anataka kuondoka Liverpool kiangazi hiki.
Manchester United imetupa ndoano kwa Raheem Sterling
Sterling akiwasili mazoezini Liverpool Jumatano jioni
Sterling atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Anfield kwenda United na kuvunja mwiko wa miaka 51 wakati Phil Chisnall alipojiunga na Liverpool 1964 akitokea Old Trafford.
Comments
Post a Comment