Free State Stars wakubali kumpa Ngassa jezi yake…



Free State Stars wakubali kumpa Ngassa jezi yake…

ngassa sauz 1

Uongozi wa Free State Stars inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini umekubali ombi la  Mrisho Ngassa kupewa jezi namba 17 ambayo amekuwa akiitumia.

Blog ya michezo ya Salehjembe amemkariri meneja wa Free State Stars, Motuba Mokoena akisema Ngassa ameomba kupewa jezi namba 17  aliyoitumia  wakati anacheza Kagera Sugar, Yanga na  Simba, na mpaka sasa anaitumia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

"Ngassa ameomba tumpe jezi na kumi na saba. Tumeona hilo linawezekana na tutalifanyia kazi.

"Naweza kusema ni uhakika tutampa jezi hiyo na kazi ya kuwakabidhi jezi mpya wachezaji wote itafanyika rasmi  leo," Meneja huyo ameiambia Salehjembe.

Tayari Ngassa yuko Afrika Kusini ambako amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne.

Baada ya kukabidhiwa jezi, leo, Ngassa ataondoka kwenda kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Cosafa inayofanyika nchini humo.



Comments