Memphis Depay ametua London kwa mapumziko mafupi na kudai atakuwa mchezaji bora duniani wakati huu anapojiunga na Manchester United.
Klabu hiyo ya Old Trafford ilitangaza kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Holland kwa pauni milioni 25 wiki iliyopita na anakuwa mkali wa kwanza wa hali ya juu kusajiliwa na Louis van Gaal msimu huu.
Depay anaweza kufikia kiwango cha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo na kuwa mwanasoka bora duniani.
"Watu wengi wananifananisha na Crtistiano Ronaldo, nafurahi kusikia hivyo, lakini wakumbuke kuwa ndio kwanza nina umri wa miaka 21, ila naamini siku moja nitafikia levo yake," alisema Depay.
Depay ametua England kwa ndege ya kukodi lakini atarejea Holland kuishuhudia timu yake ya PSV ikicheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Den Haag Jumapili hii.
Hata hivyo Depay hatacheza mchezo huo akihofia kuumia katika mechi ya kukamilisha ratiba kabla hajatua rasmi Old Trafford.
Memphis Depay baada ya kutua London
Depay (katikati anajiunga na Manchester United kwa pauni milioni 25
Depay akiitembelea England kwa mara ya kwanza na United
Depay (wa pili kushoto) akipata mlo London
Depay akipozi kwenye ngazi za ndege ya kukodi tayari kwa safari ya London
Comments
Post a Comment