David De Gea amewaacha mashabiki wa Manchester United nyoyo zao zikidunda kwa kasi baada kuonekana akikwea pipa kuelekea Madrid Jumatatu mchana.
Kwa muda mrefu wa msimu huu, kipa huyo amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Real Madrid.
De Gea ambaye alisaini kujiunga na United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid, amepewa mapumziko hadi Jumatano hii katika mpango wa kocha Louis van Gaal kukipumzisha kikosi chake.
Kipa huyo ameamua kutumia mapumziko hayo mafupi kurejea nyumbani kwao Madrid, safari ambayo imezua wasiwasi mkubwa kwa mashabiki wa United.
De Gea anatajwa kama mtu anayesakwa na Real Madrid kuchukua nafasi ya kipa veterani Iker Casillas.
Inaaminika De Gea mwenye umri wa miaka 24 ameanza kuwa na njozi za kurejea nyumbani ingawa ameendelea kuwa kimya kwa muda mrefu na kuichanganya United ambayo imekuwa ikihangaika kumsainisha mkataba mpya.
David De Gea (katikati) ameenda Hispania kufuatia mapumziko mafupi waliyopewa wachezaji wa Manchester United
De Gea (kulia) amekuwa akihusishwa na Real Madrid
Iker Casillas nafasi yake Real Madrid inazidi kuyoyoma
Comments
Post a Comment