Kwa namna yoyote ile, huu ni msimu mwingine wa mafanikio kwa Cristiano Ronaldo. Magoli 61 katika mechi 54 kwa Real Madrid, kuchukua tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya tatu katika maisha yake, taji la UEFA Super Cup na taji la FIFA Club World Cup, si mafanikio madogo.
Ni kwa hali kama hiyo ndiyo inayomfanya Ronaldo asisite kujirusha na kufurahia maisha baada ya msimu kumalizika licha kuambulia nafasi ya pili ya La Liga, kutolewa kwenye nusu fainali katika Champions League na kutupwa nje kwenye kombe la mtoano la Hispania (Copa del Rey).
Picha zifuatazo zinamuonyesha Ranaldo akiwa kusini mwa Ufaransa akiponda raha ufukweni na washkaji zake.
Cristiano Ronaldo akifurahia jua la ufukweni
Ronaldo akipozi kwenye boti kusini mwa Ufaransa
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 akila raha na marafiki zake
Comments
Post a Comment