CHELSEA YAMNASA NATHAN KINDA WA BRAZIL MWENYE UMRI WA MIAKA 19 ...mwenyewe athibitisha kupitia Instagram
Chelsea imefanikiwa kumsajili kinda wa maajabu kutoka Brazil baada ya mchezaji huyo Nathan kuthibitisha mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Dogo huyo ambaye alifikisha umri wa miaka 19 mwezi Machi, alifika London mwezi uliopita kwaajili ya mazungumzo ya usajili huo pamoja na kufanya vipimo vya afya.
Bado hakuna taarifa rasmi kutoka Chelsea, lakini jana usiku Nathan aliweka picha Instagram akithibitisha safari yake ya kwenda Stamford Bridge akitokea Club Atletico Paranaense.
katika kushibisha picha hiyo, Nathan akaandika "Ndoto imetimia" huku pia akiishukuru klabu yake ya Club Atletico Paranaense aliyoichezea kwa miaka sita.
Hii ndio picha aliyotupia Nathan Instagram kuthibitisha safari yake ya kujiunga na Chelsea
Nathan kuvaa uzi wa blue msimu ujao
Comments
Post a Comment