West Brom imepata ushindi wa kuduwaza dhidi ya Chelsea kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England ambapo hadi mwisho wa mchezo mabingwa wakawa wemalala 3-0.
Kama vile hiyo haitoshi, kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas akalimwa kadi nyekundu ya kijinga katika kipindi cha kwanza baada ya kumpiga na mpira Chris Brunt kufuatia mzozo uliomuhusisha Diego Costa.
Mabao ya West Brom yalifungwa na Saido Berahino dakika ya 9 na 47 huku lingine likifungwa na Chris Brunt dakika ya 60.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akaitumia mechi hiyo kuwaonjesha utamu wa Ligi Kuu makinda wake wawili Nathan Ake na Izzy Brown.
Makinda hao walioingizwa dakika kumi za mwisho za mchezo hawakuwa na chochote cha kubadili sura ya mchezo.
West Brom: Myhill, Dawson, McAuley, Olsson, Lescott, Brunt, Fletcher, Yacob, Morrison (Baird 89), McManaman (Gardner 54), Berahino (Ideye 79)
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Loftus-Cheek (Ake 73), Matic, Remy (Brown 79), Fabregas, Hazard, Diego Costa (Cuadrado 64)
Kipa wa Chelsea Courtois akiruka bila mafanikio kuzuia shuti la Berahino
Berahino anashangilia moja ya mabao yake katika mchezo dhidi ya Chelsea
Fabregas akilimwa kadi nyekundu
Comments
Post a Comment