Chelsea imeanzisha maongezi na Radamel Falcao pamoja na wawakilishi wake ili kuangalia uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Colombia kutua Stamford Bridge.
Falcao alichemsha katika msimu mzima alioitumikia Manchester United kwa mkopo akitokea Monaco ambapo alifunga magoli manne tu katika mechi 29 alizocheza.
Kocha wa United Louis van Gaal alithibitisha wiki iliyopita kuwa hawana mpango wa kumpa mkataba wa kudumu Faclao ambao ungeigharimu klabu hiyo ya Old Trafford pauni milioni 44.
Hata hivyo uwepo wa Falcao hapo United umeigharimu timu hiyo kiasi cha pauni milioni 40 kuanzia mshahara wake wa pauni 285,000 kwa wiki na ada ya pauni mil 6 ya kumchukua kwa mkopo.
Inaaminika Falcao yupo tayari kupunguza mshahara wake na tayari alishawaamuru wawakilishi wake wamtafutie timu nyingine ya Premier League.
Wakala wake Jorge Mendes amesema zipo dalili ya mteja wake kutua Stamford Bridge. Jorge Mendes pia ndiye wakala wa kocha wa Chelsea wa Chelsea Jose Mourinho.
Nahodha wa Colombia Radamel Falcao akikabidhiwa bendera na Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos siku ya Ijumaa
Falcao huenda akatua Chelsea
Comments
Post a Comment