Carlos Tevez anasemekana kuwa mbioni kurudi katika Premier League huku akiripotiwa kuichagua Liverpool kuwa kituo chake kipya.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City, Manchester United na West Ham anaaminika kujiandaa kufunga virago kuondoka Juventus kiangazi hiki.
Ingawa hivi karibuni alitupilia mbali taarifa kuwa anataka kuondoka Turin, gazeti la Telegraph limeripoti kuwa staa huyo anazingatia ofa ya kujiunga na Liverpool.
Hata hivyo wataalam wa mambo wanaona suala la Liverpool kukosa nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao linaweza kuwa kikwazo kwa Tevez.
Kuondoka katika timu iliyoingia fainali ya Ligi ya Mabingwa na kwenda kujiunga na timu iliyokosa nafasi ya Champions League ni tatizo.
Comments
Post a Comment