Carlo Ancelotti amefungiwa hadi msimu unapoisha.


Carlo Ancelotti amefungiwa hadi msimu unapoisha.

carlo-ancelotti-real-madrid-valencia-liga-bbva-05092015_1smwusbvm2o1l1dg7tse2h8ups

Na anwar Binde.

Kocha wa timu ya Real Madrid atakosa michezo yote iliyobakia ya msimu huu baada ya kufungiwa na shirikisho la soka la uhispania {RFEF}.

Kufungiwa huko kunahusishwa na makofi ya dharau aliyompigia refa wa mchezo kati ya Real Madrid na Valencia waliotoka sare ya goli 2-2 jumamosi iliyopita.

Ancelotti alikutwa na makosa hayo baada ya kuvunja sheria ya kifungu namba namba 117 ya nidhamu ambayo inasema "kwa wote ambao watashughulika na waamuzi awe meneja au maafisa wengine kwa hali yoyote ile awe na hasira au mitazamo ya dharau au kupuuza … adhabu yao ni kusimamishwa " .

Mwamuzi Carlos Clos Gomez aliandika katika ripoti yake ya mchezo" Mwisho wa mchezo kocha ancelotti kutoka umbali wa mita 30,aligeuka na kunipigia makofi ambayo ni ya dharau na yanapingana na maamuzi yangu  katika mchezo ule"

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 atakosa mechi hizo hadi msimu huu unaisha dhidi ya Espanyol na Getafe,katika harakati za kupunguza pengo la pointi 4 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Barcelona.

Real Madrid wanakutana na Juventus leo katika usiku wa ulaya na kujaribu kubadili matokeo ya 2-1 baada ya kupoteza mechi ya kwanza,Barcelona tayari wameshafuzu kwa fainali ya juni 6 pale Berlin.

 



Comments