Brad Friedel Kutundika Daluga msimu Huu ukiisha


Brad Friedel Kutundika Daluga msimu Huu ukiisha

brad-friedel-tottenham-hotspur_3009413

Friedel , 43, aliingia Uingereza mwaka 1997, kujiunga na majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool lakini pia amezichezea Blackburn, Aston Villa na Tottenham Hotspur anayoichezea hivi sasa kama golikipa.

Kama Muamerica huyo atacheza mechi yoyote ya Spurs kati ya mbili zilizobaki msimu huu basi atakuwa ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia kuwahi kucheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League)

Brad Friedel ni moja kati ya makipa watano tu katika Ligi Kuu ya Uingereza kuwahi kufunga goli. Wengine ni Paul Robinson, Peter Schmeichel, Asmir Begovic na Tim Howard.

"Najivunia sana kwa nilichovuna katika kazi yangu"  Alisema, "Siku nilipoanza safari yangu sikufikiri kama ingekuwa ndefu hivi"

Friedel, ambaye atatimiza miaka 44 mnamo tarehe 18 Mei, alisema atakumbuka ile hali ya mazoea ya kila siku aliyokuwa nayo kwa wachezaji wenzake na wafanyakazi wa klabu.

Aliongeza, "Siku yangu ya kutimiza miaka 44 imefika (inakaribia) kwa hiyo nadhani ni muda muafaka wa mimi kupumzika"

Friedel anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi mfululizo katika Ligi Kuu – mechi 310, kati ya Agosti 2004 na Novemba 2012 – pia ni moja ya makipa watano tu waliofunga goli kwenye Ligi Kuu.

Alijiunga na Spurs mwaka 2011 na kwa sasa tayari anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wao mwenye umri  mkubwa zaidi. Lakini hajacheza mechi yoyote msimu huu, mechi yake ya mwisho kucheza ilikuwa ni Novemba 2013.

Endapo Friedel atacheza dhidi ya Hull City au Everton katika mechi mbili za Spurs zilizobaki kwenye Ligi Kuu, hiyo itamfanya  ampite kipa wa zamani wa Manchester City, John Burridge ambaye ndiye anashikilia rekodi ya kucheza mechi ya Ligi Kuu akiwa na umri mkubwa zaidi, miaka 43 na siku 162.

"Nimekuwa na wakati mzuri sana hapa na nimekutana na watu wengi wakubwa pia katika safari yangu" aliongeza Friedel, ambaye ameichezea timu ya mpira wa miguu ya Marekani (USA) mechi 82. "Hii ni klabu nzuri sana ya mpira wa miguu na najihisi kuheshimika kuwa sehemu yake kwa miaka minne"

Friedel amepanga kumalizia masomo yake ya ukocha ili apate leseni yake ya juu ya ukocha (Pro-Coaching Licence)  pia atakuwa akifanya kazi katika vituo vya habari na lingine ni kuwa balozi wa klabu yake ya Tottenham.



Comments