Dejan Lovren
MLINZI wa Liverpool, mwenye umri wa miaka 25, raia wa Croatia, Dejan Lovren jana ame-post picha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akionesha sura yake ilivyochubuka.
Lovren ameonesha sehemu iliyochanika juu ya jicho lake la kulia na inahitaji kushonwa kwa nyuzi nne.
Mbali na sehemu hiyo, Lovreno pia ameonekana kuwa na baadhi ya alama za michubuko sehemu nyingine ya uso.
Lakini beki huyo ameshindwa kumtaja mchezaji mwenzake aliyesababisha ajali hiyo akiishia kuuliza ' kisia ni nani?"
Lovren amekumbwa na wakati mgumu katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu England baada ya kujiunga Anfield kwa paundi milioni 25 akitokea Southamptom majira ya kiangazi mwaka jana.
Wekundu hao wa Anfield wanaikaribisha Crystal Palace jumamosi ya wiki hii kabla ya kucheza mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Stoke.
Ona picha ya Dejan Lovren hapo chini;
Comments
Post a Comment