Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana                akicheza mpira pamoja na marafiki zake mjini Bujumbura                licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.
            Rais                    Nkurunziza,alikuwa akisakata kabumbu ndani ya mji mkuu                    wa Bujumbura mji uliokumbwa na maandamano makubwa                    tangu atangaze nia ya kuwania awamu ya tatu uongozini.
            Hii                  leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja                  amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.
            Mtu huyo alikuwa                    miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais                    Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.
            Walioshuhudia                  wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi                  mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama                  ngome ya upinzani.
            Waandamanaji                    walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura                    lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa                    machozi.
            Rais                  wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia                  laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo                  katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani.
            Katika                  hotuba kwenye runinga ya taifa, amesema kuwa asilimia                  tisini na tisa nukta tisa ya Burundi ina amani.
            Anasema                  kuwa hakuna mtu yeyote anayetaka kufufua taharuki ya                  kikabila.
            
Comments
Post a Comment