BAYERN MUNICH YALIPA KISASI KWA BARCELONA LAKINI 'KURA' HAZIKUTOSHA ...yaaga Champions League kwa bao 5-3, muuaji ni Neymar
Bayern Munich imelipa kisasi kwa Barcelona baada ya kuitandika 3-2 kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini bado haikuwa tiba ya wao kusonga mbele.
Kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 3-0, Bayern imeaga michuano kwa jumla ya magoli 5-3 huku Barcelona sasa ikisubiri mshindi kati ya Real Madrid na Juventus katika mchezo utakaochezwa jumatano usiku.
Mehdi Benatia alikuwa wa kuwanza kuifungia Bayern Munich dakika ya saba lakini Neymar akachomoa dakika ya 15 kabla hajaongeza la pili dakika ya 29.
Robert Lewandowski akaisawazishia Bayern dakika ya 59 huku mshambuliaji Thomas Mueller akiwapa wenyeji goli la tatu dakika ya 74.
Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi wakishangilia
Mehdi Benatia akiifungia Bayern boa la kwanza
Neymar anachomoa bao
Neymar anamzidi ujanja Jerome Boateng na kuifungia Barcelona bao la pili
Comments
Post a Comment