Linaitwa Kombe la Mfalme na Mfalme amefanya mambo yake. Leo Messi amefunga moja ya mabao yake bora kabisa katika maisha yake soka na kuisadia Barcelona kutwaa kombe hilo la mfalme (Copa del Rey) katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Atheltic Bilbao.
Katika fainali hiyo iliyopigwa Camp Nou Jumamosi usiku, Messi akapangua mabeki wanne kabla ya kufunga bao litakalobaki kuwa kumbukumbu isiyofutika. Hilo lilikuwa goli la kwanza la mchezo lillokuja ndani ya dakika 20 za mwanzo.
Neymar akafunga bao la pili dakika ya 36 na kufanya washindi waende mapumziko wakiwa wanaongoza 2-0.
Ulikuwa ni usiku wa Messi kwani dakika ya 74 aliifungia Barcelona bao la tatu kabla ya Williams hajafunga goli la kufutia machozi kunako dakika ya 79.
Kwa mtaji huo ni wazi kuwa Messi anakwenda kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Balon d'Or) mwishoni mwa mwaka huu, ambayo itakuwa ni mara yake tano kufanya hivyo.
Lionel Messi akikimbia kushangilia boa lake maridadi
Messi akiwapangua mabeki na kufunga bao la ajabu
Neymar (katikati) akishangilia goli lake
Neymar anakunja ngumi kushangilia wakati Barcelona ikipata goli la pili
Messi akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya Barcelona kupata bao la tatu
Comments
Post a Comment