MSHAMBULIAJI Jeryson Tegete na kiungo Nizar Khalfan wamesajiliwa na timu mpya iliyopanda ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, Mwadui fc.
Kocha mkuu wa Mwadui, Jamhuri Musa Kihwelo 'Julio' amethibitisha kuwasajili wachezaji hao waliotemwa na Yanga na kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Julio amesema bado anaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji wengi wenye uzoefu ili ligi ikianza kikosi chake kiwe na makali ya kutisha.
Comments
Post a Comment