BAADA YA KUMNASA DEPAY, MANCHESTER UNITED SASA YATENGA PAUNI MIL 45 KUMSAJILI HARRY KANE WA TOTTENHAM

BAADA YA KUMNASA DEPAY, MANCHESTER UNITED SASA YATENGA PAUNI MIL 45 KUMSAJILI HARRY KANE WA TOTTENHAM
Manchester United imepania kuhakikisha mshambuliaji nyota wa Tottenham, Harry Kane  anatua Old Trafford msimu ujao na kuvaa uzi mwekundu.
Kocha wa United Louis van Gaal ameainisha majina kadhaa ya wachezaji anaowataka baada ya kuirejesha klabu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Van Gaal anataka kununua mshambuliji wa kati sambamba na kuimarisha sehemu ya beki wa kulia, sentahafu na kiungo mchezeshaji.
Akiwa tayari ameshamnyakua winga Memphis Depay  kutoka PSV, Van Gaal anaelekeza nguvu zake kwa Kane ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza wa Tottenham kufunga mabao 30 kwenye msimu mmoja baada ya mkongwe Gary Lineker.
Kane ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na nusu mwezi Februari anatarajiwa kuigharimu Manchester United zaidi pauni milioni 45. 
 Manchester United boss                  Louis van Gaal is prepared to spend big on hot shot                  Harry Kane
 Manchester United boss Louis van Gaal is prepared to spend big on hot shot Harry Kane
Kane has already featured in                  the promotional shots for Tottenham's new home kit
Kane has already featured in the promotional shots for Tottenham's new home kit
Spurs fans would have been                  hoping to see him wearing the new 2015/16 shirt next                  season
Spurs fans would have been hoping to see him wearing the new 2015/16 shirt next season

Comments