Azam fc yawatia kitanzi Morris, Mourad


Azam fc yawatia kitanzi Morris, Mourad

aggrey-morris_14gnz6lfrmx2k1p7zc8h6ko0bs

KAMA kuna timu ilikuwa inawakodolea macho mabeki wa kati wa Azam fc, Said Hussein Mourad na Aggrey Morris kitumbua kimeingia mchanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kufanya maamuzi ya haraka.

Siku chache baada ya ligi kuu  msimu wa 2014/2015 kumalizika, Azam imekaa chini na kutafakari kwa kina, hatimaye imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja Mourad ambaye alikuwa huru toka aprili 16 mwaka huu.

Katikati ya mwezi aprili mwaka huu, Morad kupitia mtandao huu ulitangaza kuwa huru na alikaribisha ofa kutoka timu yoyote, lakini alisema anaipa muda timu yake ya Azam kwani bado anahitaji kufanya nayo kazi.

Hatimaye mawazo yake yamekamilika na msimu ujao ataendelea kuvaa uzi wa Wanalambalamba.

Aggrey Morris ni beki mahiri ndani ya Azam na Taifa Stars, hivyo makamu bingwa hao wa ligi kuu wameamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.

Tangu kusajiliwa kwa Paschal Wawa dirisha dogo la usajili mwezi desemba mwaka jana, Aggrey amekuwa akicheza vizuri na beki huyo wa zamani wa El Merreikh ya Sudan.



Comments