Ni moja ya fainali nyepesi kabisa kuwahi kutokea! Arsenal imefanikiwa kutetea taji lake la FA kiulani kabisa baada ya kuifunga Aston Villa 4-0.
Katika fainali hiyo ya FA iliyopigwa kwenye uwanja wa Wembley, hadi mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Theo Walcott dakika ya 40.
Kipindi cha pili Arsenal walicharuka zaidi na kupata magoli mengine matatu yaliyofungwa na Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 62 na Olivier Giroud dakika ya 90.
Per Mertesacker akishangilia bao lake na lililoifanya Arsenal iongoze 3-0 dhidi ya Aston Villa kwenye fainali ya FA Cup
Theo Walcott akiifungia Arsenal boa la kwanza
Beki wa Villa Alan Hutton (kushoto) akishindwa kuzuia mchomo wa Walcott lililozaa bao la kwanza
Mkwaju mkali wa Walcott ukijaa wavuni
Walcott akishangilia goli lake
Arsenal: Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil (Wilshere 76), Sanchez, Walcott (Giroud 76)
Aston Villa: Given, Hutton, Okore, Vlaar, Richardson (Bacuna 67), Cleverley, Westwood (Sanchez 70), Delph, N'Zogbia (Agbonlahor 52), Benteke, Grealish
Comments
Post a Comment