Inasemekana Arsenal wamewasiliana na            familia ya Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund kwaajili ya usajili wa            kiangazi kijacho.
        Ripoti kutoka Ujerumani zinasema Arsenal            na Atletico Madrid wamekuwa wa            kwanza kubisha hodi wakati Manchester            United, Bayern Munich na Manchester City zikichukua tahadhari kutokana na rekodi ya            majeruhi ya kiungo huyo.
        United kwa sass imeamua kutohangaika na            usajili wowote hadi msimu utakapoisha.
        Irfay baba wa Gundogan ndiye            wakala wa mwanae lakini Dortmund wamesisitiza kuwa            hawajapokea ofa yoyote.
        Ilkay Gundogan (kulia)              anawaniwa na timu kubwa za Ulaya
        Gundogan anajiandaa              kutimka Dortmund 
        
Comments
Post a Comment