ARSENAL YALA KIPORO KILICHOOZA, YAPIGWA 1-0 NA SWANSEA ...nafasi ya pili sasa hatarini, ya tatu nayo mashakani
Arsenal imeshindwa kutumia vizuri mchezo wake wa kiporo cha Premier League baada ya kulambwa na Swansea 1-0.
Bafetimbi Gomis aliifungia Swansea bao pekee zikiwa zimebakia dakika tano mpira kumalizika, akimalizia kwa kichwa krosi ya Jefferson Montero.
Bao hilo lilisaidiwa na teknolojia mpya ya goli baada kipa David Ospina kufanikiwa kuokoa mpira lakini ikabainika kuwa tayari ulishavuka mstari wa goli.
Arsenal sasa watakwenda Old Trafford Jumapili wakiwa na tahadhari kuwa kupoteza mchezo huo kunaweza kuwafanya wawe nyuma ya vijana wa Louis van Gaal.
Ingawa bado watakuwa na mchezo mmoja mkononi, lakini Arsenal watakuwa kwenye presha kubwa na iwapo watateleza basi nafasi ya tatu itakuwa mashakani, achilia mbali nafasi ya pili.
Kikwazo kikubwa kwa Arsenal kilikuwa ni kipa wao wa zamani Lukasz Fabianski ambaye aliondoa michomo mingi ya wazi ikiwemo ya Alexis Sanchez na Theo Walcott.
Siku zote Arsene Wenger alikuwa akiamini kuwa Lukasz Fabianski ni kipa bab kubwa na usiku huo wa Jumatatu mlinda mlango huyo akadhirisha hivyo.
Fabianski aliondoka Arsenal kiangazi kilichopita licha ya Wenger kujitahidi kadri awezavyo kumshawishi abakie Emirates.
ARSENAL (4-2-3-1): Ospina 6; Bellerin 6, Mertesacker 6, Koscielny 6, Monreal 6; Coquelin 6 (Wilshere 60, 6), Cazorla 6.5; Ramsey 6.5, Ozil 6, Sanchez 6; Giroud 5 (Walcott, 6).
Manager: Arsene Wenger 6.
SWANSEA (4-1-4-1): Fabianski 8; Rangel 6 (Richards 60, 5), Fernandez 6.5, Williams 6.5, Taylor 6; Cork 6.5; Dyer 6 (Barrow), Shelvey 6, Ki 6 (Gomis), Montero 6; Sigurdsson 5.
Kipa wa Arsenal David Ospina akijaribu kuokoa mpira Bafetimbi Gomis ulizaa goli dakika ya 86
Referee Kevin akionyesha kuwa hilo ni goli baada ya kubainika kuwa mpira ulivuka mstari
Mshambuliaji wa Kifarasan Bafetimbi Gomis akishangilia bao baada refa Kevin Friend kuthibitisha kuwa ni goli
Ni goli, hakuna ubishi
Lukasz Fabianski akiondoa moja ya hatari
Lukasz Fabianski akisalimiana na kipa wa akiba wa Arsenal Wojciech Szczesny baada ya mchezo
Comments
Post a Comment