ARSENAL YAANZA MDOGO MDGO KWENYE USAJILI, YANASA WAWILI KUTOKA UFARANSA ...ni eff Reine-Adelaide na Yassin Fortune wa Lens
Arsenal imefikia makubaliano na klabu ya Lens ya Ufaransa kwaajili ya kuwasajili machipukizi wake wawili Jeff Reine-Adelaide na Yassin Fortune.
Wachezaji wote wawili ni washambuliaji ambao pia wana uwezo wa kucheza kama viungo na wote waliiwakilisha Ufaransa kwenye michuano ya kimataifa ya U 17.
Daily Mail linaandika kuwa Fortune alikuwa anatakiwa na United lakini timu hiyo ya Old Trafford ikabwaga manyanga baada ya kutajiwa bei.
Lens imewauza wachezaji wote wawili kwa pauni milioni 3 pamoja na marupurupu kutokana na namna watakavyokuwa wakicheza kwenye kikosi cha kwanza.
Reine-Adelaide na Yassin Fortune wataungana na Yaya Sanogo ambaye alihamia Emirates Stadium baada ya kung'ara Ufaransa.
Hata hivyo Sanogo ameshindwa kufurukuta England, Arsenal ikamtoa kwa mkopo kwenda Crystal Palace ambako nako ameshindwa kung'aa.
Arsene Wenger anawaongeza Jeff Reine-Adelaide na Yassin Fortune kwenye kikosi chake
Fortune (kushoto) na Reine-Adelaide (kulia) wanatua Arsenal kwa pauni milioni 3
Reine-Adelaide na Yassin Fortune wataungana na Yaya Sanogo ambaye alihamia Emirates Stadium baada ya kung'ara Ufaransa.
Comments
Post a Comment