Andre Schurrle arudishwa Chelsea kuvaa medali, Torres akosa vigezo!


Andre Schurrle arudishwa Chelsea kuvaa medali, Torres akosa vigezo!
3,w=559,c=0.bild
Ni kawaida kwa kila bingwa wa ligi kuu England kuwa na namna yake ya kusherekea ubingwa wake, hivyo Chelsea nao wapo katika mipango madhubuti ya kufanya tukio hilo kubwa.
Klabu na wasimamizi wa ligi wanakaa chini na kupanga sherehe za ubingwa ambazo zitajumuisha wachezaji watakaopewa medali.
Kama unavyojua kwa Chelsea, kuna wachezaji walikuja  katikati ya msimu na wengine waliondoka, hivyo klabu inatakiwa kupiga hesabu ni wachezaji gani wana sifa ya kuvaa medali na ambao hawatavaa.
Mchezaji angalau anatakiwa kuanza kikosi cha kwanza katika mechi tano (5) za ligi kuu ili kukidhi kigezo cha kuvaa medali-kwahiyo Fernando Torres amekosa sifa kwasababu alianza mechi moja tu kabla ya kupelekwa kwa mkopo mwezi wa nane mwaka jana.
Andre Schurrle aliuzwa katika klabu ya Wolfsburg wakati wa dirisha dogo la mwezi januari mwaka huu, lakini alianza  mechi 9 katika nusu msimu alioichezea Chelsea, hivyo Mjerumani huyo ana vigezo vya kuvaa medali.
Akihojiana na John Bennett wa BBC, nyota huyo tayari  amethibitisha kuwa Jose Mourinho amemtaarifu kurudi London kuvaa medali.
Some ujumbe huu hapa chini;



Comments