Ancelloti atilia wasiwasi kibarua chake msimu ujao


Ancelloti atilia wasiwasi kibarua chake msimu ujao

carloancelotti

Kocha wa Real Madrid, Rai wa Italia, Carlo Ancelotti  sasa amekuwa na matarajio ya kutopata au kupoteza kibarua chake kuifundisha Real Madrid.

Akizungumza kupitia kituo cha Sky Sports mapema baada ya filimbi ya mwisho, Ancelotti alisema

" Sijui, tuna siku 15 sasa kwaajili ya maandalizi ya mechi 2 zilizobakia za ligi kisha tunamaliza msimu na kisha mazungumzo na klabu yatafuatia".

" Suala la kuongelea hatima yangu na klabu sio la kujadili hivi sasa, inabidi tumalize msimu vizuri iwezekanavyo" alizidi kusema.

"Tulipoteza katika mchezo wa awali, wachezaji wetu walicheza vizuri sana lakini hatukuwa na bahati, tulifanikiwa kupata nafasi nyingi sana lakini tulikosa kuzitumia"

" Ni vigumu kusema, timu ilifanya kila kitu kilichopaswa kufanyika, tukishambulia sana lakini hatukuwa na bahati, kama ni kujilaumu basi ni ile mechi yetu ya awali kule Turin"

" Mpira ni maelezo madogo, mwaka jana tulishinda na tunashukuru kwa goli la dakika za mwisho na kila mtu alisema ilikuwa bahati na hatua hii hatukuwa na bahati kabisa ila yote kwa yote najisikia vyema juu ya wachezaji hawa"

Katika mchezo huo pia kiwango cha Gareth Bale bado hakikuwa kile kizuri kama ilivyozoeleka pindi anapokuwa yupo na ari nzuri ambapo Ancellot hakusita kumzungumzia na akisema

" Alicheza vizuri, alijituma sana kwa bidii kama timu nzima ilivyofanya, tulionesha kile tulichokiandaa lakini haikuwa nafasi yetu ya kufika fainali" Muitaliano huyo alisema.



Comments