HAPPY BIRTHDAY STEVIE WONDER, KAMA UTABAHATIKA KUELEZWA KUHUSU WEBSITE HII. Lakini leo ni birthday ya muimbaji ambaye alitunga na kuimba kati ya nyimbo bora za birthday karne hii. I just called to say I love you. Stevland Hardaway Judkins alizaliwa May 13, 1950, jina lake analotambuliwa kisheria ni as Stevland Hardaway Morris, Stevland alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita wa Calvin Judkins na mkewe Lula Mae Hardaway. Stevland alizaliwa njiti, alizaliwa wiki sita kabla ya muda wake na hivyo akalazimika kuwekwa katika mashine ili kumuwezesha kuishi, jambo ambalo liliathiri macho yake hivyo pamoja na kuwa alizaliwa akiona alipofuka muda mfupi baadae wakati bado mdogo. Alianza kupenda muziki akiwa bado mdogo sana na akiwa na umri wa miaka 11 tu kipaji chake kiligunduliwa na mwanamuziki Ronnie White wa kundi la Miracles, pamoja na umri wake muda mfupi baadae aliweza kuingia mkataba wa kutengeza muziki na kampuni kubwa ya Motown Records. Akapewa jina la jukwaani la Little Stevie Wonder. Stevie ni kati ya wanamuziki wanaoheshimika duniani kote kutokana na utunzi uimbaji upigaji wa vyombo na hasa Keyboards. Wimbo wake Fingertips uliingia katika Billboard Hot 100 akiwa na miaka 13, na hivyo kumfanya msanii mdogo kuliko wote aliyewahi kuingia katika chart hizo. Stevie ana Grammy 25 mpaka sasa.
Happy Birthday Stevie Wonder miaka 65 si mchezo.
Comments
Post a Comment