Alichosema Ngassa baada ya kumwaga wino Free State ya Afrika kusini


Alichosema Ngassa baada ya kumwaga wino Free State ya Afrika kusini
11165069_927757313933469_6640690287012942628_n
"Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu (Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza soka ya Tanzania, ili klabu zisijifikirie tena kusajili wachezaji wa Tanzania,"amesema Ngassa asubuhi ya leo nchini Afrika kusini baada ya kusaini mkataba wa miaka 4 kuichezea timu ya Free State inayoshika nafasi ya 9 katika ligi kuu nchini humo.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba amekuwa akimpenda Ngassa kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo siku moja. 

 



Comments