Kesi ya kufanya mapenzi na msichana chini ya miaka 16 inayomkabili mshambuliaji wa pembeni wa Sunderland, Adam Johnson katika mahakama ya mwanzo ya Dorham Crown imeahirishwa mpaka juni tatu mwaka huu, huku akiachiwa huru kwa dhamana.
Johnson amewasili mahakamani akiwa na mpenzi wake leo baada ya kushitakiwa kwa makosa matatu ya shughuli za ngono na moja la kukaa kinyumba na msichana chini ya miaka kumi na sita.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, leo amethibitisha tu jina lake, tarehe ya kuzaliwa, anuani yake na kuieleza mahakama kama anayafahamu mashitaka yake.
Katika dakika tano za kusikilizwa kwa kesi yake, Wakili wa Johnson, Paul Morris ameonekana kuwa na shauku ya kuisihi mahakama isimtie hatiani mteja wake.
Johnson ambaye ameichezea England mechi 12 alitiwa mbaroni mwezi machi mwaka huu baada ya kutuhumiwa kufanya makosa hayo mwezi januari, wakati kosa la kuishi kinyumba na msichana mdogo lilitokea kati ya mwezi desemba na februari mwaka huu.
Tangu kutiwa mbarano, Johnson aliyeanzia maisha yake ya soka katika klabu ya Middlesbrough ameichezea Sunderland mechi sita .
Comments
Post a Comment