Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Yanga wanakabiliwa na mechi ngumu ya kimataifa dhidi ya Etoile itakayochezwa Tunisia siku ya wafanyakazi dunia mwaka huu.'
WAMESHTUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu ya Yanga kuamua kusitisha sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2014/15 ili kujiandaa vyema kwa ajili ya mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile Sportive du Sahel (ESS).
Yanga SC, timu kongwe zaidi VPL msimu huu, jana ilitwaa taji la 25 la Tanzania Bara na inatakiwa kusafiri kwenda Tunisia kuwakabili mabingwa hao wa zamani wa Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa barani Afrika katika mechi ya marudiano iliyopangwa kuchezwa Mei Mosi nchini humo.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jery Muro, ameuambia mtandao huu jijini hapa leo mchana kuwa wameamua kusitisha sherehe za ubingwa hadi pale watakaporejea kutoka Tunisia.
"Tumeamua kusitisha zoezi hilo la sherehe za ubingwa mpaka tutakaporudi kutoka Tunisia maana timu iko kambini," amesema Muro.
Yanga itatumia ndege ya biashara kwenda Tunisia. Haitatumia ngege ya rais waliyopewa kwenda Zimbabwe kuikabili FC Platinum.
Comments
Post a Comment