BOMOA TUTAJENGA KESHO- Orchestra Mambo Bado, Mtunzi -Tchimanga Assossa
WOTE- Bomoae Bomoae Bomoa mama tutajenga kesho imaa, Tujajenga kesho imaa x2
JENIFA NDESILE-Imaao enyi watoto wazuri wote, njoni tucheze leo bomoa
WOTE- Bomoae Bomoae Bomoa mama tutajenga kesho imaa, Tutajenga kesho imaaa
ASSOSSA- O betu bayai yoyoyo bomoa
WOTE- Bomoae Bomoae Bomoa mama tutajenga kesho imaa, Tutajenga kesho imaaa
SOLO GITAA

ASSOSSA-Kumbe njoni wote tucheze bomoa
WOTE- Kumbe njoni wote tucheze bomoa
ASSOSSA- O betu bayai yoyoyo bomoa
WOTE- Bomoae Bomoae Bomoa mama tutajenga kesho imaa, Tutajenga kesho imaaa
Wimbo huu ulipitia mkasa mkubwa wa kupigwa marufuku na Umoja wa Vijana MIAKA YA 80, na hivyo kuzuiwa kupigwa redioni. Hakukutolewa maelezo kwa wanamuziki waliohusika, japo ilisemekana kuwa unahamasisha watu kubomoa wakati nia ilikuwa kujenga nchi. Wimbo huu ambao haukuwa na maudhui yoyote ya kisiasa ulipokuwa unatungwa , bali ilikuwa ni jibu la mwenye ukumbi wa Lango La Chuma, baada ya wanamuziki kumwambia kuwa siku watazindua ukumbi, utajaa mpaka ubomoke. Wimbo ulikuwa katika awamu ya kwanza ya nyimbo zilizorekodiwa na bendi ya Orchestra Mambo Bado mwanzoni mwa miaka ya 80. Na Bomoa ilikuwa ndio staili ya uchezaji show wa bendi hii, wacheza show wakiwa ndio waliokuwa maarufu wakati ule, akina Pangapanga, Chileshi Ally, Stella na Nadhifa.
Bendi hii ilikuwa chini ya uongozi wa Tchimanga Assossa ambaye ndie alikuwa muimbaji na mtunzi mkuu. Wimbo huu ulikuwa na washiriki wafuatao. Tchimanga Assossa, George Mzee, John Kitime, Lucas Faustin na msichana pekee Jenipher Ndesile ndio waliimba, Huruka Uvuruge Solo gitaa, William Masilenge rhythm gitaa, Likisi Matola Bezi gitaa, Andre Milongo gitaa la Solo la pili, Sadi Mnala Drums.
Comments
Post a Comment