Arsenal imeripotiwa kuweka mezani ofa ya uhamisho wa pauni milioni 11.8 kwa mshambuliaji wa Roma ya Italia, Mattia Destro ili kumpa changamoto Olivier Giroud.
Kwa mujibu wa gazeti la Forza, bosi wa Gunners, Arsene Wenger alikuwa na nia ya kumpeleka Emirates staa huyo wa kimataifa wa Italia tangu misimu michache iliyopita.
Destro kwa sasa anacheza kwa mkopo AC Milan baada ya kujiunga nayo Januari, lakini timu hiyo ya Serie A haina mpango wa kumpa mkataba wa moja kwa moja.
Comments
Post a Comment