Kuna uwezekano Wayne Rooney akakosa mechi mbili zijazo za Manchester United kutokana na kuumia goti na kuna hofu hataweza kucheza tena msimu huu.
Kukosekana kwa nahodha huyo aliye kinara wa mabao wa United litakuwa pigo kubwa kwa matumaini ya timu hiyo kuwabwaga wapinzani wao Liverpool katika vita ya kuwania nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao.
Rooney aliyeumia goti baada ya kugongana na mchezaji mwenzake Ander Herrera katika mechi waliyoshindwa nyumbani kwa Everton Jumapili iliyopita taarifa inaeleweka kwamba tathmini ya awali inapendekeza kukaa nje kwa wiki mbili.
Hiyo itamfanya akose mechi ya nyumbani dhidi ya West Brom Jumamosi na ya wikiendi inayofuata nyumbani kwa Crystal Palace. Lakini kama hali yake itashindwa kutengemaa mapema, Rooney anaweza pia kukosa mechi ya nyumbani dhidi ya Arsenal na siku ya mwisho watakapowafuata Hull.
Comments
Post a Comment