Wanachama Toto Africans wachachamaa!



Wanachama Toto Africans wachachamaa!
KIKOSICHATOTOAFRICAN
BAADHI ya wanachama wa Toto Africans ya jijini Mwanza wameorodhesha majina na kuweka saini wakiambatanisha na barua na kuupelekea uongozi wa klabu hiyo wakimtaka Mwenyekiti kwa kushirikiana na kamati ya utendaji waitishe mkutano mkuu wa dharula ufanyike tarehe 3/05/2015 kujadili masuala ya msingi yanayoitatiza klabu hiyo.
Ajenda zinazotajwa ndani ya barua hiyo ni pamoja na Taaarifa ya fedha msimu wa ligi hatua ya pili ya ligi msimu 2013-2014 na msimu wa 2014-2015.
Mkataba wa kisheria na mdhamini (Nsejjere)
Kujiuzuru kwa viongozi muhimu wa Klabu (Mwenyekiti na wajumbe wawili)
Ukiukwaji wa Mamlaka ya Utendaji na kupelekea uvunjwaji wa katiba ya Toto African, pia sekretarieti kushindwa kusimamia majukumu yao kwa kipindi chote.
Mpango mkakati wa ushiriki ligi kuu pamoja na kuunda kamati za kufanikisha malengo ya ushiriki na kadhalika. 


Comments