WACHEZAJI MANCHESTER UNITED WAHOFIA DE GEA KUTIMKIA REAL MADRID


WACHEZAJI MANCHESTER UNITED WAHOFIA DE GEA KUTIMKIA REAL MADRID

Mastaa wa Manchester United wanahofia kwamba kipa wao namba moja, David De Gea ataondoka Old Trafford na kujiunga na Real Madrid.
Kipa huyo raia wa Hispania amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake nab ado hajasaini dili jipya Old Trafford licha ya juhudi za bodi ya United na kocha Louis Van Gaal.
Madrid inamtaka kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 kwenda kuchukua nafasi ya Iker Casillas.
Gazeti la Daily Mirror limedai kuwa wachezaji wa United wamemshawishi kipa huyo anayetaka kuondoka baada ya miaka minne. 
Kama De Gea atatangaza nia ya kuondoka, United inaelezwa kuwa itaikamua Madrid pauni milioni 50.


Comments