Ukweli wa ajabu: Pep Guardiola anashinda taji kila baada ya mechi 18



Ukweli wa ajabu: Pep Guardiola anashinda taji kila baada ya mechi 18
CDii_NbWMAAqlp7
JE, PEP Guardiola ndiye kocha bora zaidi duniani?
Ilikuwa wikiendi nzuri kwa Bayern Munich jana jumapili baada ya Borussia Monchengladbach kushinda 1-0 dhidi ya Wolfsburg na kuwapa ubingwa rasmi The Bavarians.
Kama ilivyoripotiwa na @Squawka, Pep Guardiola sasa ameshinda mataji matano kati ya 6 aliyoshiriki akiwa kocha: Matatu na Barcelona na mawili akiwa na timu yake ya Bayern.
 @MisterChiping ameeleza mwanzo mzuri wa Pep: Pep Guardiola ameshinda makombe  19 katika mechi 348 alizoongoza timu ( mechi 247 akiwa na Barca na mechi 101 akiwa na Bayern), na hii inamaanisha kwamba Mhispania huyo ameshinda taji kila baada ya mechi 18.
Ukweli mwingine wa Takwimu: Guardiola ameshinda idadi ya makombe (19) katika miaka 7 sawa na alivyofanya kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal aliyeshinda idadi hiyo kwa miaka 24 ya ukocha wake na Sven Goran Eriksson aliyeshinda idadi hiyo hiyo ndani ya miaka 35 ya kufundisha soka.
Mwisho, Guardiola ameshinda makombe 19 kati ya 27 aliyoshindania katika maisha yake ya kufundisha soka na kumfanya awe na mafanikio ya asilimia 70.
Bado rekodi ya Pep inaweza kuongezeaka kwasababu ana uwezekano wa kushinda makombe mpaka 21 kati ya 29.


Comments