Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Plujim (kulia)
RUVU Sootings na Yanga zitachuana kesho katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mechi ya raundi ya kwanza iliyopigwa januari 17 mwaka huu uwanja wa Taifa, timu hizo zilitoka suluhu (0-0).
Hiyo ndio mechi pekee ambayo Ruvu Shooting hawakuruhusu goli katika mechi 9 walizokutana kwa mwaka wa tano sasa (kuanzia 2010).
Kipigo kikubwa zaidi Ruvu Shootings kupokea kutoka kwa Yanga ni magoli 7-0 msimu uliopita.
kocha mkuu wa Yanga sc, Hans van der Pluijm amewaongoza vijana wake katika mazoezi yaliyofanyika asubuhi ya leo uwanja wa Karume Dar es salaam na amesema: "Tuko tayari kwa mechi, tunajua kila mechi ni ngumu kwetu, unapohitaji kuwa bingwa unahitaji kushinda kila mechi iliyopo mbele yako. Tuko tayari kushinda ili tubakishe pointi tatu za kutupa ubingwa".
"Cannavaro (Nadir Haroub) hayupo fiti kucheza kesho, siku zote siongelei wachezaji wasiokuwepo kwenye programu yangu. Yanga ina wachezaji zaidi ya 25 na wate wanaweza kutumika".
Yanga inaongoza ligi kuu ikijikusanyia pointi 49 baada ya kushuka dimbani mara 22, ikifuatiwa na Azam fc yenye pointi 42 katika nafasi pili baada ya kucheza mechi 22.
Comments
Post a Comment